Coke Studio kwenye muziki wa kisasa

Coke Studio ni bonge la kipindi kinacho kuletea mfululizo wa misimu yenye makala tofauti na ya kusisimua kwa wapenzi na wadau wa muziki duniani kote.

Coke Studio

Tokea kuanzishwa kwa kipindi hiki wasanii wengi wamepata shavu na kung’aa kwenye soko la muziki na burudani kwani Coke Studio inachukua nafasi ya kwanza kukuza talanta miongoni mwa vijana wengi.

Kwa sasa imefikia msimu wake wa Nane ( Season 8) huku wakiwa na takribani 45 epsodes jambo linaloleta fahari kwa sababu Coke Studio hukutanisha pamoja wasanii wa aina mbalimbali ya nyimbo kutoka sehemu tofauti za dunia ikwemo Kenya.

Wasanii wengi Afrika wamehusika kwenye Coke Studio hii ya kifahari kwa ajili ya kurekodi nyimbo zao kwa ushirikiano na wasanii wengine. Nchini Kenya msanii Victoria Kimani kutoka Chocolate City, Avril, na wengine kutoka Nigeria, Mr. Flavour na wengine maarufu duniani kama Ne-Yo wa Marekani.

Ushirikiano huo maarufu kama Mash up uleta upendo na amani kwani wasanii uweza kuona uwezo wa wasanii wenzao wanaofanya muziki wa R&B, Bongo Flava, Genge, Reggae, Dancehall, Rock miongoni mwa nyingine nyingi na kutayarishwa na producer  Strings kwa ajili ya kupeperushwa kwenye runinga.

Kwa hiyo wasanii wanajiunga kwa asilimia kubwa zaidi kwa sababu ya kuondolewa kwa ada ya kujiunga na Coke Studio na kwa sasa ni bure bilashi. Bahati Kenya ni msanii anayefanya muziki wa ‘Gospel’ inakisiwa kujiunga humo hivi karibuni.

Ili kujua zaidi kuhusu Coke Studio na pia kuskiliza nyimbo zao bonyeza link ifuatayo.

http://cokestudio.com.pk

Advertisements