Koffi Olomide baada ya Kenya huyo Zambia

Udhalilishaji na ukandamizaji wa haki za binadamu hususan wana wake na watoto ni kitu kinachokiuka katiba ya Kenya.

Mkali wa Rhumba kutoka Demokrasia ya Congo alizua timbwili hali ya tafrani katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta nchini Kenya.

Koffi Olomide alionekana mtovu wa nidhamu wakati alinaswa kwenye camera akimpiga teke mmoja wa wadada aliyowasili nao kwa minajili ya kutoa bonge la burudani kwenye ukumbi wa Bomas of Kenya jumamosi iliopita na kusema alikusudia kumzuia mwanamke aliyekuwa akimshambulia dansa wake huyo.
Gwiji huyo alirejeshwa nchi DRC siku hio ya Jumamosi na madansa wake wa kike baada ya mamlaka za Kenya ya wanarika na jinsia kupinga show yake kutokana na utundu wake.

Koffi mwenye umri wa miaka 60 imesemekana kuwa yeye ni mtu mwenye fujo kwani anadaiwa kumdhalilisha Producer wake kwa kumpiga ‘Kiki’ mwaka 2012 na kuhukumiwa jela kifungo cha nje cha miezi mitatu.Pia alimvunjia kamera mwanahabari wa kituo cha TV cha RTSA huko DRC.
Hata hivyo mwimbaje huyo ameelekeza ziara yake ya kufanya shows nchini Zambia anakotegemewa ku perform tarehe 30, 31 na Agosti 1. Hii imethibitishwa na waandaaji wa Show hio ya Koffi kupitia wizara ya Kilimo na Biashara. Kulikuwepo tetesi kuwa show hio kafutiliwa mbali.

Advertisements