Koffi Olomide na majanga tu

Majanga yanazidi kumuandama gwiji wa muziki wa Rhumba kwani angali anazuiliwa magerezani.

Koffi Olomide- Gwiji wa Rhumba

Antoine Christophe Agbepa Mumba anayetamba kwa jina Koffi Olomide alifikishwa Mahakamani siku ya Jumatatu wakati alipokamatwa na Polisi kwenye maskani yake jiji la Kinshasa DRC.

Olomide alikanusha mbele ya jaji tuhuma zinazomkabili za kumpiga teke na kuhujumu haki za binadamu alipotua uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta nchini Kenya wakati alipokuja kufanya tamasha. Alinaswa kwenye Kamera haki mdhalilisha mnenguaji huyo wa kike.

Kwa mujibu wa wakili wake Olomide amenyimwa kulipa dhamana yoyote aachiliwe huru  na jaji.

Gwiji huyo mpaka sasa anakadiria hasara baada ya tamasha zake kufutiliwa mbali Kenya na ile ya Zambia.

Koffi ana umri wa miaka 60 (sitini) kwa sasa.

Koffi Olomide

Advertisements