Otile Brown Moto wa kuotea mbali

By: Julius Jumah.

Otile Brown

Kwa vitu ambavyo mwenyezi Mungu kamjaalia kando na ufundi wa mashairi ya kimziki yenye maudhui komavu ni sauti isiyo kifani.Otile Brown, mwenye mizizi ya uswahilini na aliye chini ya uongozi wa Dreamland music inayoongozwa na Dr.Eddie anatarajiwa kutoa shipa jipya Jumatatu tarehe kumi Agosti. Nyimbo hii inakwenda kwa jina #PAKATE na amewahakikishia mashabiki wake kuwa ni moto wa kuota kama umejistiri kwa friji.

Otile Brown


Mkali huyu ametamba na nyimbo kama Dejavu ambayo remix yake aliwashirikisha wasanii Papa Jones, Sudi Boy na mwigizaji Abel Mutua. Alivyonipenda aliyomshirikisha King Kaka pia imenoga na inapigwa kila sehemu. Kibao chake kinachotamba kwa sasa ni Basi audio na video vikifanywa na Dr. Eddie.

Tutarajie yepi kutoka kwa mkali huyu? Tupia maoni yako.

Advertisements