Kristoff Bifu na King Kambongosi

Kwa siku kadhaa zimepita kumekuwa na fununu kuhusu bifu Kati ya wakali hawa wa Hip Hop wanaofanya vizuri katika game ya muziki Kenya.

King Kambongosi ambaye ameanza kung’aa kupitia ngoma yake kali “Yapapala” ambayo inatesa anga za burudani amesema kuwa anaskia fununu za kutishiwa maisha na Kristoff Kenya aka mluhya wa busia ambaye ngoma yake mpya “Gudi Gudi” inapenya vizuri kwenye vituo vya habari na mitandao.

Kristoff Kenya


Kwa mujibu wa Kambongosi anayetambulika kwa jina la Sanaa KamaThe Luhya King Rapper ni kuwa kuna mtu asiyefahamika  alitumwa kuleta vitisho hivyo kwenye studio ya Track Lab ambayo anarekodia Kambongosi.
Kwenye gumzo na King Kambongosi alisema kuwa Kristoff hapendi kuskia kwamba kuna King ambaye anawakilisha jamii ya Waluhya kwa jumla kupitia muziki wenye asilia ya Kiluhya kwani yeye inaonekana kuwa anawakilisha sehemu Fulani ‘Busia’ kwa muziki wake wenye wingi wa Kiingereza.

Mambo na kuvunjana Aina maana watu huvunjana Kwa mic” aliongeza kwa kusema kwamba “Na mi I’m King of Western not muluyha wa busia“.


The Luhya King Rapper naye kwa upande wake anadai kuwa hataki mgogoro na Mluhya wa Busia na yuko radhi kushindana naye kimuziki kupitia Mic lakini sio kuvunjana kwa gumi kwani haisaidii kusuluhisha bifu hio.
Mkali wa ‘Niko Fiti’ inadaiwa kuwa anataka wafanye collabo ya wawili wao ili kumaliza tafrani hii tofauti na hivyo kuvunjana tu.

Kristoff Kenya

Mkazivaeunit

Advertisements

2 responses to “Kristoff Bifu na King Kambongosi

  1. it will be best if the both guys talk coz a true musician does his or her stuff focusing his or her audience but not doing it targeting to create biff with other artists.artsts need to be themselves and do stuffs that will be educating the citizens but not doing them to attack other artist

    Liked by 1 person

Comments are closed.