Dazlah ahusika kwenye ajali Likoni

Siku ya jana tarehe 8/8/2013 msanii maarufu nchini Kenya alihusika kwenye mkasa mbaya wa ajali ya barabarani.

Dazlah Kiduche

Taarifa kutoka mwambao wa pwani ni kwamba msanii kwa nyimbo za kizazi kipya anaetamba kwa hiti kwa jina UCHOYO aliyoshirikiana na Sis P, Dazlah amepata ajali barabarani pamoja na dada zake wawili. Meneja wake hit maker wa Kidekide, Produza Tee amesema ndugu hao watatu walihusika katika ajali jana Jumatatu, tarehe nane Agosti 2016 maeneo ya Likoni.Wote hao wamesafirishwa hospitalini kwa matibabu ikisemekana kuwa Dazlah alipata majeraha mepesi kichwani huku dada zake wakiwa katika hali mbaya.

Wote walikuwa kwenye Tuk Tuk wakielekea mjini Mombasa walipogongana gari ndogo.

Dazlah


Kwa sasa wamelazwa hospitali ya Likoni kwa ajili ya matibabu.
Sisi kama familia ya Mkazivae Unit tunawatakia afueni za haraka. Pamoja tuwakumbuke katika sala zetu.

Mkazivaeunit

Dazlah

Advertisements