Mpango mzima wa Timu Wcb Wasafi huu hapa

Dah! Msafiri ni aliye bandarini manake Wcb Wasafi wameweka mambo yao hadharani.


Huku tukihesabu siku tu mkali “Kidogo” Diamond Platnumz kudondoka mji wa Meru Kenya kufanya makamuzi ya ajabu tarehe 27/8/2016 tamasha ambalo nimeandaliwa na kampuni ya Watanashati Classic Entertainment, vijana wake ambao wamesainishwa kwenye lebo hio ya Wasafi watakuwa tayari kushuka Kenya kufanya matamasha mawili tofauti katika mji wa Lodwar tarehe2/9/16 na katika mji wa Mombasa tarehe 3/9/2016.

Itakuwa wiki ya burudani tele kutoka kwa Wcb Wasafi huku wakiongozwa na ‘Simba’. Rayvanny (Natafuta Kiki), Rich Mavoko (Acha Ibaki Story) na Harmonize (Matatizo) watakuwa kwenye Microphone.

Baada ya hapo Diamond anategemea kusafiri hadi jiji la Los Angeles Marekani kwenye Show take huko tarehe 2 mwezi October kisha adondoke nchini kwako Tanzania tarehe Mosi mwezi October kuanza matamasha ya nyumbani Tanzania.

mkazivaeunit

Advertisements