New video: “KONFAM”  Van so da Gamma ft Naiboi & T’dat

Siku ni leo jumanne tarehe 27/9/2016 ambapo shipa kali likiambatana na  kichupa linadondoka.

Van so da Gamma


Mkali wimbo “Juu ya Doh” amerudi upya kuteka hisia za mashabiki na wadau wa muziki mzuri lakini pia kutesa industry ya muziki Afrika Mashariki tena.

Van so da Gamma msanii anayezidi kukita mizizi kwenye game ya muziki Kenya kwa mara hii kaamua kuwapa shavu wakali hawa, Timmy T’dat na The Naiboi wa Pacho Entertainment kwenye ngoma yaitwa “Konfam”(Confirm).

Kwenye mchongo na Van so, amefunguka kusema kuwa aliibuka na idea ya wimbo huo ambao una ujumbe maalum kwa wanajamii kuwa waangalifu wanapojikuta wakitekeleza jambo au nyakati za maamuzi magumu kwani kuna maovu yanayotokea katika jamii zetu.

Van so da gamma


Bonge la wimbo #Konfam limetayarishwa na Jack on the beat/ Cedo Pacho Studio na kuongozwa na Crystal Prime Mtumina.
Tafadhali nami nakusihi tu Konfam na pia share hii link.

BRAND NEW MUSIC VIDEO!! KONFAM – VANSO DA GAMA X TDAT X NAIBOI

mkazivaeunit


Advertisements