Chris Brown na Wizkid Mombasa Kenya

Chris Brown & Wizkid


Lisemwalo lipo na kama halipo laja. Baada ya kusambaa tetesi na uvumi kwamba mkali wa hip hop na RnB kutoka America atafanya show Kenya limethibitika.
Baada ya Trey Songz msanii wa marekani kuwepo Kenya kwa ajili ya maandalizi ya show ya kurekod ‘Coke Studio Africa’ mwezi huu wa kumi, msanii mwengine mkali atatua mji wa Mombasa kufanya makamuzi ya kiutu uzima.

Chris Brown


Chris Brown amethibitisha kuja Mombasa kwa ajili ya show hio Jumamosi hii tarehe 8/10/2016 itakayofanyika katika Mombasa Golf Club. Tamasha hili la aina yake linaandaliwa na Mombasa Rocks pamoja na serikali ya kaunti ya Mombasa.
“Yoyo 001, Mombasa Kenya, can’t wait to come

out there. Kenya we are turning it up. October 8th

make sure you’re there, make sure you’re ready

and we are gonna party, thank you.” alithibitisha Chris Brown.

Gavana wa kaunti hiyo Hassan Joho amepania kufanya mjio huo makao makuu ya muziki na burudani na kubadilisha sura ya Mombasa.

Hata hivyo kitu cha kufanya wengi kutokwa na jasho ni kiasi cha fedha ambacho kinaumiza vichwa vya wengi. Tiketi ya kawaida (Regular) 6,000, (VIP) 20,000 na (VVIP) 50,000. zinapatika kwa Jambolife.com huku mwisho wa kuchukuwa tiketi ni Jumatano.


Mkali huyo wa ‘Loyal’ na ‘Sweet Love’ na ambaye anatamba na album yake mpya “Royalty” atatoa bonge la burudani kwenye stage moja na mkali wa ‘Sound It’ Wizkid lakini pia wasanii wengine wa Kenya na Tanzania.
TUKUTANE MOMBASA

mkazivaeunit


Advertisements