Fahamu nini Coke Studio Africa  wanakuletea wewe

Get Ready for this year’s big event.


Kampuni ya Coca cola inapenda kukukaribisha wewe na wenzako kutazama msimu wa nne wa makala ya Coke Studio Africa kupitia television yako.
Coke Studio season 4 na ambacho ni kipindi babkubwa duniani kinachowakutanisha wasanii wa aina tofauti kwenye Sanaa, wanahakikisha wanaibua na kukuza talanta za vijana wengi mitaani.

Makala haya ya nne ambayo yanafanyika hapa Nairobi Kenya, yamekwisha andaliwa tayari kabisa kupeperushwa kwenye TV tarehe 9/10/2016 Jumapili.

Majuzi tu tumeshuhudia msanii mwimbaji gwiji kutokea Marekani,Trey Songz humu nchini kwa ajili ya maandalizi hayo kwani atakuwa Guest Artist Surprise.

Hata hivyo msimuj huu umekuwa na mabadiliko kwani hata mataifa husika yamezidishwa mengine sita na kufikia mataifa 11. Hapa ni Ivory coast, Cameroon, Ghana,DRC, Senegal na Ethiopia ndio yameongezeka.

Mbali na mataifa pia wasanii wapya wamepata shavu msimu huu kuonyesha uwezo wao Kama vile (Nigeria) Kiss Daniel na Patoranking. (Uganda) Eddy Kenzo na Radio & Weasel. (Togo) Toofan. (Ethiopia) Haile Roots. (Kenya) Bahati Kelvin.

Bahati Kelvin


Wasanii wengine ambao walikuwepo kisha wakazama ila wamerejea ni pamoja na: 2Baba(Nigeria), Vanessa Mdee(Tanzania).
Kwa ufupi msimu huu tunashuhudia mabadiliko mengi mpaka kwa maproducers wa kipindi hiki. Kusudi kuweza kuonyesha utaofauti na pia ubora wa utendakazi. Kama Una kipaji usikimwe kwame. Jitokeze uwahi Bahati yako. Sauti Sol na The Kansol watakuwepo.

Madraxx ndiye producer kutoka kenya kashirikishwa kwenye Coke Studio Africa season 4.

mkazivaeunit


Advertisements