Raila,Joho,Kiba kwenye show ya Chris Brown

Muziki ni kitu huwezi kuepuka maishani mwako hata kama una inda na msanii husika.

Taarifa za ujio wa mkali wa Hip Hop na RnB Marekani kutua Kenya tayari kutumbuiza kwenye tamasha la #Mombasa Rocks Festival zimefanya maelfu ya mashabiki kufurika mji huo kuona wakali wa muziki jukwaani.

Kiongozi wa mrengo wa Cord Msh.Raila Odinga hakuachwa nyuma kuhudhuria tamasha hilo pamoja na gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho pamoja na msanii Ali Kiba. Kwa mujibu wa picha aliyoitulia kwa Facebook yake Raila wakifurahia mazingira mazuri ya pwani.

Joho, Raila & Kiba


Kwenye tamasha hilo la Leo usiku Jumamosi ya tarehe 8/10/2016, mwimbaji Vanessa Mdee amethibitisha uwepo wake jukwaani kutokana na tetesi za awali kwamba waandaji wa show hii walishindwa kufikia matakwa yake. Msanii huyu wa ‘Niroge’ ataupamba mji wa Mombasa kwa mbwembwe zake kwani ni mara yake ya kwanza kutumbuiza humo. Ameshiriki kuandika wimbo mpya wa kundi la South Africa Mafikizolo.


Hali hiyo ya mushkili iliweza kusuluhishwa na gavana Joho. V money alimshkuru gavana huyo.

Hatimaye msanii atakaye teka mji wa Mombasa aliwasili nchini na tuhuma zinamzingira kwamba alipasua simu ya shabiki mmoja alipojaribu kupiga picha ‘Selfie’ na yeye alipotua uwanja wa ndege.

Kama ilivyotokea wakati wa mwimbaji DRC Congo Koffi Olomide, kwa kuzua fujo uwanja wa ndege JKIA na kushurutisha wakenya kumkinai na kumfanya arejeshwa kwako kupitia jumbe za mitandaoni, pia mori na hasira za wakenya zimebainika kwa kutuia #DeportChrisBrown.
Lakini pia hakuna ushaidi wowote kwenye camera zilizonasa tukio hilo la Chris Brown kulingana na taarifa za awali za kituo cha NTV Kenya.


Atakuwa akipanda jukwaani kwa kusindikizwa na wasanii kama vile; Wizkid, Navio, Nazizi na Vanessa Mdee.
mkazivaeunit


Advertisements