“Msanii Yeyote anaweza kurekodi WCB Wasafi” amesema Lizer

Kwa sasa kuna lebo nyingi duniani zinazoshughulika na muziki na kumilikiwa na watu maarufu.

Afrika Mashariki kuna wasanii watajika wenye studio zao binafsi za kurekod muziki. Wasanii kama Bob Junior, Proff. Jay, Jaguar KE, Diamond Platnumz miongoni mwa wengine.

WCB Wasafi ambayo inamilikiwa na msanii Diamond, imekuwa iking’aa kwa muda sasa tangu kuanzishwa na kusainisha wasanii kama Rich Mavoko, Harmonize, Rayvanny na wengineo.

Producer Lizer


Inadaiwa kuwa studio hio haichukui wasanii wa nje kurekodi humo ila hizo ni tetesi tu kwani madai hayo yamethibitishwa na Producer kwa jina Lizer kutok Wasafi Records kwamba msanii yeyote anaweza kurekodia hump kwa hela yake tu.
“kama studio zingine wanavyofanya nasi

tunafanya hivyo hivyo pia. Msanii mwingine

yeyote kutoka sehemu yoyote anaruhusiwa kuja

kurekodi hapa. Hatuna bei kubwa sana bei yetu ni

ndogo sana ukizingatia na studio ilivyo kubwa

lakini bei yetu ni ndogo sana,” alisema Lizer.

Hatuo hii imetokea kwa kuona ukaribu wa wasanii kama Dully Sykes, Shetta na Chege wakitumia lebo hio katika kazi zao za sanaa.

mkazivaeunit

Advertisements