Msanii Msomi kutokea Meru Amecharuka Kinoma

Sasa kama hujafahamu kuwa uwezo ulionao hakuna yeyote anaweza kukupongeza pata ushauri kwa msanii huyu.

Gabby Wema


Anaamini kuwa yeye ndiye shabiki wa kwanza wa kazi zake za sanaa hata kama kuna wanaodharau.

Gabby Wema


Gabby Wema mwimbaji wa Bongo Flava kazaliwa 1995 na kukulia katika familia ya kawaida huko Meru County. Amekuzwa na mama yake Mzazi na sasa ni msanii msomi anayetarajia kuhitimu chuo mwezi Disemba kama Public Health Officer.
Gabby Wema alijitosa katika ulingo wa muziki na burudani mwaka jana alipoachia Kibao chake cha kwanza ‘Ningekuwa na Uwezo’ katika Hos Studio Malindi.

Gabby na Marafiki zake


Hata hivyo Gabby amefanya kazi na Ceaser kutokea C & G studios mtayarishaji ambaye alimwandalia track mbili ‘Ngoja Kukicha na Kwa Sala’.
Kwa sasa Gabby anarekodi kwa Producer Tharmos Wa GrandPa Records.

Japo kuwa muziki una changamoto na pesa nyingi huja mwisho wa safari, Gabby amekiri wazi kuwa anapenda muziki muda wote na kama hasikilizi nyimbo, anatunga nyimbo.

Gabby


Mwimbaji huyo wa ‘Kwa Sala’ ameweka nyimbo zake kwa mtandao wa mdundo.com unaweza kupakua na kuskiliza kwa YouTube video yake ‘Ningekuwa na Uwezo’.
Kwa Sala na Ngoja Kukicha bado hazina videos.

TUSAMBAZE UPENDO UKIPATA NAWE SHARE HII..

mkazivaeunitmkazivaeunit.wordpress.com

Advertisements

2 responses to “Msanii Msomi kutokea Meru Amecharuka Kinoma

Comments are closed.