Auditions za Fimbo Ya Nne kutoka GrandPa Records ndio sasa

Imefika ule muda Wa kufahamu lebo kubwa Afrika Mashariki inatuandalia nini mwaka huu.

​Kila mwaka GrandPa Records huwa tayari kuachia wimbo kwa kukuunga wasanii wengi kwa single Moja maarufu kama Fimbo.

Baadaya ya kuachia Fimbo ya tatu, uongozi mzima unajipanga kuja upya na style mpya itakayo teka anga za burudani East Africa.

Refigah


Nimepiga gumzo kwa kina na kiongizi wa lebo hio Refigah aka Heviweit na kunidokezea kuwa raundi hii Fimbo ya Nne ni moto kwani itakusanya vipaji change na magwiji wa muziki pamoja kutoka kanda ya Afrika Mashariki nzima.
“Eeh ni kweli Fimbo ya nne ipo njiani na matayarisho ndo yanaendelea. Tunafanya auditions za wasanii mbalimbali wakubwa na wachanga kwenye game.” aliendelea kusema kuwa “Sio Kenya pekeake bali ni wasanii kutoka East Africa nzima ili kuleta ladha tofauti” amesema Heavyweight.


Majaribio ya kwanza jiji la Nairobi yemekwisha kufanywa tayari. Tusubiri tuone wapi pengine.

mkazivaeunit

Advertisements