KISA CHA MKAZIVAE

Huh ni mfululizo wa hadithi fupi kuhusu chimbuko (kisa) cha jina Mkazivae.

(1).Kisa Cha Mkazivae

Jumamosi moja kuntu jua lilichomoza kama kawaida na kuleta nuru ya kutafuta maisha mema hususan kwa wanadamu. Kukakucha kulichele hali ya kufanya kila kiumbe che uhai na  uwezo wa kutambaa, au kupuruka, kuchupa, na kutembea kufanya jambo hima kusaka riziki.
Ndivyo ilivyo kwamba kwenye watu hakukosi umbea kama sio maneno ya Baraka kukuombea. Nilipiga guu mosi guu pili baada ya shughuli zangu za kuweka nyumba safi na pia kukidhi matakwa ya tumbo langu, nikaelekea afisini.

​Kisa cha jina Mkazivae, kilijiri pale pale ofisini kwa bwana Keesi, nilipokuwa kwenye Internship au masomo ya nyanjani katika kufanikisha stashahada yangu ya kozi ya Uanahabari katika chuo mawasiliano Kenya Institute Of Mass Communication mwaka wa 2014. Hapa nikuwa Nyanjani mji wa Machakos (KNA) pamoja na wenzangu wanazuoni kwenye shughuli hio.

Kwa kawaida masela zangu tulipenda sana kuchokoza, kufurahia maisha, kutangamana na watu na pia kujifunza mapya ya magazetini. Jembe langu mmoja asubuhi hio alibisha mlangoni hapo akiwa na baadhi ya magazeti kiganjani iwemo Mwanaspoti.

Dogo huyo anapenda story za game utadhani naye nduguye Mourinho mkufunzi wa klub ya Manshester United jopo ni shabiki ya Chelsea Fc.

Alianza, “Dogoo Leo nina Mwanaspoti, nachambua story zote hapa kisha ndo nikupe hili gazeti, sawa? Mimi bila ubishi wala nini nikakubaliana yae kwani ndiye kaleta gazeti. ” Safi Mwanetu”. hapo hapo nikamjibu.

​Masela wenzetu walikuepo afisini kila mmoja bize na magazeti ya kiingereza kusaka yaliyojiri ili kujifahamisha kama kawida ya mwanahabari. Dogo huyo tulizoea kumwita jina ‘Mwanetu’ ilivyosheria za wasahili wa visiwani.

Punde tu alipoanza kulichambua gazeti, Mwanaspoti, alikumbana na kisa chenyewe. Alifunua ukrasa wenye picha za wanamichezo yaani wana kabumbu fulani kutokea jiji la Mombasa kwa mujibu wa Mwanaspoti. Ghafla akanionyesha picha hio ilotiwa maandishi kwa kifupi tu ‘Nendeni Mkazivae’!!

Hapo hapo tukafunga safari ya kwenda kusaka habari za kuchapisha magazetini au kutangzwa radioni. Tukafululiza hadi sokoni, hatukukaa masela wakashauri twendeni tukapunge hewa sehemu za mbali kidogo.

​Tukazivaa viatu tukazifunga kisawaswa, tukafunga ofisi hapo hapo mpaka baadae. Tulipokuwa njiani, mambo yalipamba moto, story za anasa, kuhusu madem wazuri wazuri, vicheko vya furaha na shibe ya asubuhi, tukakosa kulihisi jua kali.Mwanetu alikumbuka kisa cha ‘Mkazivae’ na kucheka kwa Furaha aliponiona nakaza mwendo kuelekea nisikokufahamu ila wao tu….

Advertisements