Ray Vanny Kutoa Ngoma Yake Mpya Na Diamond

Hivi majuzi wakali wa muziki wa bongo flava Diamond Platnumz, Alikiba na Navy Kenzo walishinda tuzo za Hippio Music Awards huko Uganda. 

Moja ya tuzo alizoshinda Diamond ni tuzo ya Video bora East Africa kupitia video ya Salome aliyomshirikisha msanii wa label yake, RayVanny aka Raymond.

Baada ya ushindi huo, Raymond amefunguka kuhusu kufanya tena ngoma na Diamond ambapo amedai kuwa itakuwa ni ngoma yake yeye. 

“Lazima,watu wasubiri,” amesema Ray kupitia Supermega ya Kings Fm.

Tayari Rich Mavoko na Harmonize Tz wamemshirikisha bosi wao huyo kwenye nyimbo zao, ‘Kokoro’ na ‘Bado’

#Mitego_Sasa 

Advertisements