Tambala kufungua Radio yake ‘Angaza Fm’

Vijana na ubunifu ndiyo nguzo kuu ya maisha ya sasa. 

Je unamfahamu kijana mmoja mwanahabari na mtangazaji maarufu Kenya? Basi habari njema ni kwamba amepania kufungua kituo chake cha radio nchini Tanzania.

Anthony Tambala

​

Anthony Tambala, ndilo jina lake kijana huyo machachari ambaye anauzoefu mpevu katika masuala ya utangazaji kwani amehudumu katika radio zaidi ya kumi na moja (11) zikiwemo Tv.

Vituo vya radio kama vile Chemichemi Fm, Radio Sahara, Radio Furaha kutaja baadhi yake tu. Hata hivyo ashakuwa kiongozi wa vituo vya radio lakini pia ni producer mkali.

Kwa sasa Tambala mwenye umri wa miaka (26),ameamua kutamba na kufungua kituo chake cha radio Geita nchini Tanzania.

Dhumni kubwa la kusogeza kituo hicho bongo, ni kwa ajili ya kujiajiri na kuwapa motisha vijana wanaopania kuwa watangazaji mahiri bongo nafasi kubwa katika kituo chake, angaza fm.

Hata hivyo Mitego_Sasa imepiga gumzo na bw.Tambala na kunyoosha haya;

“Napania kufungua Radio yangu ‘Angaza Fm’ Tanzania mwezi Wa sita. Kutakuwa pia na tuzo za wasanii nataka kuwasainisha” alisema Tambala.

Lake Zone Awards

​
Tuzo hizo kwa Lake Zone Awards zinalenga kuwapa nafasi wasanii wengi anao wasaini kupata motisha ya kufanya kazi bora zaidi na zitakuwa tayari mwezi wa sita wakati wa uzinduzi wa radio yake Angaza Fm.
#Mitego_Sasa

Advertisements