Video: Kenya Dual ft Kris Joe – ‘Acapella Lover’

Naam, muziki nchini Kenya unapaa anga za juu kila uchao kisa juhudi za wasanii wetu.

Pwani ya Kenya inajivunia vipaji hatari vya wasanii wenye hadhi kubwa pamoja na wanaochipukia. Wasanii wa pwani wamejitoa kimasomaso kurejesha heshima ya sanaa na hadhi ya wasanii huku wakilenga kupaisha muziki wetu katika ngazi za kimataifa.

Kenya Dual


Kundi la wasanii maarufu pwani, Kenyan Dual, nao ni miongoni mwa wanaharakiti. Kundi hilo linajumuisha wasanii wawili Kev(Kevin Mwenda) na Majeek( Austine Musuya) wote wanafunzi chuo kikuu cha pwani.

Kev

Kwenye umri wao wa miaka kumi na tisa (19), walijiunga pamoja kufanya muziki kwani walifahamu walikuwa na ndoto moja ya muziki japo walipania kufanya collabo mwanzoni.

Majeek


Video yao ya kwanza ilikuwa ‘Acapella Lover’ ambayo ilitesa angaza za muziki na burudani kwa kupokelewa vyema. Kisha wakaachia wimbo ‘Umeketi Na Sponsor’ ikapata mafanikio makubwa.
Kwa sasa Kenya Dual wanajipanga kuachia video yao mapema mwezi March. Chini ya miaka miwili pamoja, wamefanikiwa kuwa wasanii waburudishaji kama Live Band Kilifi kwenye Distant Relatives Lounge kila Jumapili.  Wanacheza gitaa,Wanaimba, Wanarap.

Kenya Dual, Live Band


Tazama video yao ‘Acapella Lover’ hapa;
ACAPELLA LOVER OFFICIAL BY Kenyan Dual X kris Joe..

#Mitego_Sasa_Blog

.

Advertisements