New Music: KAPNEA- ‘Nuoma’

Akiwa ni mzawa wa pwani maeneo ya Ukunda, anajivunia ubunifu wake pamoja na uzalendo mkuu.

KAPNEA


Raphael Mbwana Lugho ni mwimbaji anayekua kwa kasi sana kwenye game ya muziki Kenya. Dogo huyo maarufu kama KAPNEA jina ambalo lina asili yake kutokana na kuwa kiongozi wa mpira wa voliboli yaani Kaptain(Kap) kisha ndoto zake kuja kuwa Multimillionaire ili kuwasaidia vijana wengi kimaisha ikaleta neno (Nea). Sasa KapNea.
Msanii huyo wa aina ya muziki wa Hip Hop/Kapuka aliwahi studioni kwa mara ya kwanza ndani ya TK2 Mombasa kwa usaidizi mkubwa wa rafiki yake Jax. Hapo karekodi vibao vyake kama ‘Naongea, Ruka na Changamka’.

Punde tu mwaka wa 2016, KAPNEA alisafiri mji wa Machakos ili kuzidisha juhudi zake kimuziki alipopata shavu kwenye RedRess Records na kusainishwa. Hapo hapo akaachia wimbo wa kwanza chini ya lebo hio ‘Cheza’ ambao alisaidiwa na super producer wake Ondiko (Resoundz Media).

Kwa sasa msanii huyo anatamba na kutesa na ngoma mpya kwa jina ‘Nuoma’ ambayo ina maana ya kuwa heshimu kina dada na wanawake wote duniani kwani bila wao mambo hayaendi sawa. Wimbo huo umetayarishwa na producer Ondiko.

KEPNEA pia ni bonge la mpishi yaani   professional Chef.

#Mitego_Sasa_Blog

Advertisements