Barakah Da Prince aumbua Ben Pol

“Nilitegemea hii nyimbo itakuwa hatari. Yaani nilijua hii ngoma sijui itakuwaje kwa sababu unajua Ben Pol ni msanii mzuri,” ameongeza mkali mmoja wa bongo fleva.

Mtangazaji wa Clouds FM & Barakah

Barakah Da Prince ambaye ni mmliki wa Bana Music Records, amezungumzia ujio mpya wa Ben Paul ‘Tatu’ akisema kwamba hakutegemea msanii huyo kutoa wimbo mbaya hivyo kwa jinsi alivyokuwa akiiupa promo mpaka kuhatarisha maisha yake.

Picha ya Ben Pol

Ben Pol kabla ya ngoma hio alipost picha za utata mitandaoni huku akionyesha sehemu kubwa ya uchi wake na mikononi kufungwa, kuonyesha picha ya mtu asiye na uhuru wake katu.

Picha ya Ben Pol

 

Barakah amezungumza hayo wakati yupo kwenye kipindi XXL cha Clouds FM Tz.

“Tuache kama mimi na yeye ni marafiki, nimeongea kama shabiki na kwa sababu pia ujue kitu kama kile ujue Dozen kwa mtu kama Ben Pol karisk sana, halafu kuja anatoa nyimbo mbaya. Hapo mimi ndio nilishangaa,” Barakah amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM.

 

#MitegoEA.

Click: http://www.facebook.com/MkazivaeUNIT

http://www.facebook.com/AntonyMckenzie

http://www.instagram.com/@mc.antony

http://www.twitter.com/@antonymckenzie

Advertisements