Otile Brown anasaka kiki kwa Bahati Tena ??

Bifu la aina yake limeanza kutokota baada ya taarifa fulani kusambaa mitandaoni na kwenye media mbalimbali.

otile

Otile Brown

Inawezekana hujafahamu ujumbe aliouandika msanii kutoka pwani ya Kenya ambaye alishaingia kwenye hali ya sintofahamu na management yake ya awali  yake Dr. Eddy kutoka Dreamland Records. Mkali huyo kwa jina Otile Brown, ameonekana kurekebisha msanii wa gospel Bahati Kelvin.

Hii inatokana na collobo yake Bahati ft Eddy Kenzo wa Uganda, ‘Mama Remix’ ambapo kwa upande wake Otile haijampendeza kamwe na ameeleza wazi Bahati kwamba hio ni nyimbo mbaya sana.

bahati

Bahati Kelvin

 

Mkali huyo kwa ‘Kistaarabu‘ amemwambia Bahati kwamba atamwandikia nyimbo zake zijazo kama atahitaji msaada wake lakini pia amemshauri ajifunze jinsi ya kuweka vocals kali.

Hatua hio ya Otile imepokelewa kwa mtazamo hasi na mashabiki wake Bahati huku wakimtaka Otile aachane na nyimbo za Bahati.

Je unahisi ni vyema kwa msanii kumkosoa msanii mwenzake anapopotoka kisanaa au ni kazi ya mashabiki tu?

#MitegoEA.

Click: http://www.facebook.com/MkazivaeUNIT

Advertisements