Sky Vee kipaji kipya kutoka Kisii!!

Kwa sasa muziki nchini Kenya umeanza kuputa sura mpya na mtazamo mzuri baada ya kuona vijana wengi kutoka kaunti mbalimbali wakijikaza kinoma.

Game la muziki mara nyingi huitaji vijana wabunifu ili kuipa kiki na mwendokasi mzuri.

Kutoka kaunti ya Kisii ni dogo fulani hivi anayekua kwa kasi kwenye game, na sasa ana dude moja kali mno.

sky vee

Sky Vee ndilo jina la usanii na ameachia single audio yake ya aina ya bongo fleva kwa jina ‘Kijukujuku‘ kwa maana ya wasiwasi wa moyo wake baada ya kumlea binti moja hatimaye akavunja agano lao la mapenzi  na kumtoraka, sasa Sky Vee analia na moyo wake tu. Hiki ni kisa cha kweli kabisa!!! ameeleza msanii huyo kwenye gumzo naye.

Hata hivyo mwimbaji huyo ameweka wazi kwamba amesainishwa kwenye KG-Record lebo yake Producer Totti, Mombasa mwaka huu na ambapo ameanza kupata mafanikio ya muziki  wake.

Pata kuskiliza wimbo huo wake mpya hapa chini kwenye link:

http://Mdundo.com/a/34881

#MitegoEA

Click: http://www.facebook.com/MkazivaeUNIT

Advertisements