Video Mpya: Saida Karoli – ‘Orugambo’ 

Maisha na muziki ni kama kazi na dawa au mtu na kivuli.

Gwiji wa muziki msanii mwanadada kutoka Tanzania,na ambaye ana sifa tele kwenye game la muziki amerudi tena.

Je wamfahamu Saida Karoli aliyeimba ‘Chambua Kama Karanga’ ?Sasa mkali huyo ana kazi mpya. Saida ambaye amekulia kwa familia ya dini ya ukristo,ameachia video yake mpya ‘Orugambo’ na kufunguka mengi.

Pamoja na kujaribu kujitoa uhai mara kadhaa bila kufanikiwa, ameeleza changamoto kibao za yeye kutofanya vizuri kwenye muziki kwa kipindo kirefu.

Dada huyo ambaye anatokea katika jamii asiyoruhusu wasichana kufanya muziki, amesema kwamba ukosefu wa hela ndio chanzo kikubwa cha matatizo ya kazi yake. Saida akitoa maelezo kupitia ‘Planet Bongo’ East Afrika Radio, arikiri wazi anahitaji msaada ili afanikishe kisanaa. 

“Mimi nahitaji support ya mashabiki, wasanii wenzangu, wadau, media na kila mtu. Nikibebwa na bebeka.” asema Saida.

Pata kutazama video yake hii ambayo ameonjesha nyimbo ya Darasa, ‘ Wacha Maneno weka muziki’. Ya diamond, ‘ Wanakodoa kodo( Macho kodo)’. Kisha ya Belle 9, ‘ Give It To Me Beby’.

Saida Karoli – Orugambo ( Official Music Video ): http://youtu.be/jwAxSZblzvQ

#MitegoEA

Click: http://www.facebook.com/MkazivaeUNIT

Advertisements