Exclusive: Chanzo cha Bifu la Diamond na Kiba..

Dah! Kumbe Simba na King Kiba walikuwa washikaji kabla ya kuliamsha bifu lao?

Kwa mujibu wa mwimbaji maarufu kutokea Zanzibar, AT ni kwamba mkali hao walikuwa washikaji mno hadi walishirikiana hadi kucheza PlayStation. Sasa hapo, hapa ndio chanzo cha bifu.

“Diamond na Ali Kiba walikujaga kucheza PlayStation kwangu, siku moja Diamond akachagua Real Madrid na Ali Barcelona. Wakachezaa mara Kiba kafunga diamond, ikaendaa diamond akarejesha goli. Hapo diamond akaongeza bao la pili, naye Kiba akapata faul na hakamiss. Diamond akaongeza la Tatu”. akaeleza AT.

Hapo Ali akakasirika na kumpiga kumbo Diamond.

“Wewe mwanzo nimekutafuta sana, yaani unanitoa kwenye chart ya muziki ??” alifoka kwa hasira Kiba.

Na kwa kuwa Platnumz alikuwa mdogo wala hakuwa na mwili wa kubushana na Ali, yeye akakaa kimya licha ya kuwa alikuwa ndo mwanzo ameingia kwenye muziki.

Tangu siku hio wawili hao hawaonani jicho kwa jicho na ndo chanzo cha bifu lao.

#Mitego

Advertisements