Exclusive: Xpat Mkwanja asema alianza muziki Kanisani

Leo ndani ya ‘Count Down’ show ya Radio Maisha yake Mr.Count Down, kimeeleweka aisee!!

Clemmo na Xpat.

Clemmo 254 amepiga gumzo na Msanii mmoja matata kutokea Kisumu Kenya na kufunguka mengi kimuziki. Ni msanii aliyeanza sanaa kwenye kwaya ya kanisa kisha akabadilisha mkondo.
Xpat Mkwanja amesema yeye anafanya muziki kutokana na passion yake kwani Hata shuleni alikuwa mkali wa Poems, Mashairi na pia Hesabu. Mara nyingi anajikuta hajarekodi ngoma kwa muda mrefu hadi producer wake anamkubusha na kumtaka aachie kazi mpya. Xpat ashawahi kuwa na msanii Kush Tracey kwenye lebo moja lakini sasa Kush anafanya sole project zake lebo nyingine na pia amekuwa kimuziki.

Mwimbaji huyo wa ‘Nyama kwa Nyama’ collabo na Pro, amesema idea ya wimbo huo ni kutokana na mambo ya mtaani vijana wanapenda kuyafanya bila kuwa wangalifu.

“Wimbo huo ni kutoka kwa society inspirations. Unakuta vijana wengi wanapenda kufanya sex bila condoms Hata hawajali magonjwa, so nikapata idea ya kuwaelimisha kutumia kinga kwa mapenzi. Maradhi hapo tuwe waangalifu” yeye kamaliza hivyo.

Xpat Mkwanja  ndilo jina lake la usanii pamoja na kuwa ni mfanyabiashara. Ameweka waziki kwamba MP mteule wa eneo bunge la Starehe, Jaguar na ambaye pia ni msanii ndiye aliyemshawishi kufanya biashara kando na muziki.

“Msanii Jaguar alinipa advice kuanzisha business ili kujiendeleza” akaongea Xpat.

Kwa sasa ameachia wimbo mpya ‘Wash Wash Money’ ambao unazungumzia vijana kupata pesa za haraka zisizo za halali.

“Ngoma hio inazungumzia making fast money ambazo ni illegal. Vijana tufanye kazi na kutafuta pesa hata kama ni E-legal kwani Kenya iko digital platform” kaongezea hivyo.

#MitegoEA.

Click: http://www.facebook.com/MkazivaeUNIT

Advertisements