BAHATI,atesa sana pande za Marekani

Msanii wa muziki wa Injili Kenya amekuwa Marekani kwa ajili ya muziki wake kutafutia soko la kimataifa.

bahati

Bahati ametesa anga za muziki akiwa Marekani pindi tu baaada ya kufutilia mbali wazo la kuachana na Muziki huku mashabiki wake wengi wakimsihi aendelee na talanta yake, na sasa amerudi kwa kishindo.

Licha ya tetesi za kuachana na muziki miezi michache iliyopita, Bahati alidai kuna watu walimpangia njama za kuporomoka na kumchafulia jina kisanaa. Haya yalizua taharuki kwa wafuasi wake na pia soko la muziki wa Gospel nchini Kenya.

Ameelezea furaha yake na mafanikio anayopata kuufanya muziki wa Injili huku akizidi kumtukuza Mwenyezi Mungu.

Hizi ni picha zake akiwa Marekani..

Advertisements